- Pengine umesubiri vya kutosha ili meli ya matumaini yako iweze kutia nanga katika bandari yako bila mafanikio. Pengine ndoto yako kuu bado haijatimia. Pengine kwa kadri siku zinavyokwenda ndivyo matumaini yako yanazidi kufifia.
- Kama una uhakika na mahali meli yako iliko basi nyanyuka. Acha kuendelea kubweteka hapo bandarini kwako. Itakulazimu upige mbizi na kuifuata meli yako huko huko baharini. Kama hujui kuogelea jifunze, lakini kamwe usikae tu na kulalamika. Jifunze hatari na misukosuko ya bahari. Tunakutakia upigaji mbizi mwema !!!

No comments:
Post a Comment